- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Niwaombe watendaji wote, mnaoendelea kuchangisha michango shuleni; kuanzia leo muache kutoza michango hiyo.” Alisema Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho, wakati akitoa ujumbe wa mwenge Aprili 14, 2018 Benaco katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru Ndugu Kabeho, amesema serikali kupitia waraka wa elimu namba 06 wa mwaka 2015, ilitangaza elimu bure kwa watoto wanaosoma elimu Msingi, na waraka wa ellimu namba 03 wa mwaka 2016, unatoa maelekezo ya jinsi ya kuchangisha michango hiyo.
Hata hivyo, amesema wazazi na walezi, wanawajibika kuwanunulia watoto wao sale za shule, madaftari, kalamu pamoja na viatu kufuatana na maagizo ya shule mtoto anakosoma.
“Wazazi na walezi kwa kupitia kamati za vijiji na kata mlizounda wenyewe, mnatakiwa mchangishe michango mbalimbali, kwa ajili ya maendeleo ya shule zetu; lakini michango hii, isichangishwe na walimu.” Alisema Ndugu Kabeho.
Amewataka wazazi kuchangia maendeleo ya shule, ili michango isiathiri maendeleo ya watoto, na wala watoto wasifukuzwe shule, kwa sababu wazazi wao hawajatoa michango hiyo.
Ndugu Kabeho amesema serikali imejitahidi kuweka miundombinu mbalimbali; kama vile madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo pamoja na maabara na kuziwekea vifaa vya sayansi, ili watoto waweze kusoma kwa vitendo.
Mwenge wa Uhuru umekimbizwa wilayani Ngara Aprili 14, 2018, umeweka mawe ya msingi na kuzindua miradi saba, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili, na ulikabidhiwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Biharamulo Aprili 15, 2018.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa