- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Idara ya Ardhi Ndg Enock Mponzi Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Amesema kwamba program Mpya ya Benki ya Dunia ya kuiandaa Mipango shirikishi jamii ya matumizi ya ardhi na uboreshaji wa Usalama wa Miliki za ardhi tayari imeanza kutekelezwa wilayani Ngara kuanzia tarehe 09/12/2023.
Aliendelea Kwa kusema Mradi huo unatekelezwa na kwa kusimamiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi amesema Malengo Makuu ya Mradi huo ni kuandaa Mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vyote 75 vya Wilaya ya Ngara Aidha katika lengo hili la matumizi ya ardhi kazi zinazotekelezwa Sasa ni
1. kuhakiki na kupima upya mipaka ya vijiji vyote 75
2 . Kutenga na kupima Maeneo Kwa matumizi Mbalimbali kama vile Maeneo ya malisho, Maeneo ya vyanzo vya maji,Maeneo ya misitu,njia za Mifugo na Maeneo ya huduma za Jamii.
3. kuandaa na kusajili vyeti vya Ardhi za vijiji vyote 75
4. kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi Kwa Kila Kijiji.
Aidha alisema Hadi Sasa Mradi umeisha kamilika katika vijiji 10 Vya Mwanzo ambavyo ni Kanyinya, Mbuba, Ruhuba, Kumwendo, Mururama, Djoululigwa,Ibuga, Nyabisindu Mukarehe na Murugarama.
Aidha vijiji vingine 10 vitakavyofuatia ni Mumuhamba, Bukiriro, Kihinga, Nyarulama, Mumilamila, Bugarama, Rwinyana, Nyabihanga, Mukubu na Muganza.
Ndg. Mponzi alimalizia Kwa kusema Kwa awamu hii ya kukamilisha Mipango ya Matumizi Bora ya ardhi wamepanga kukamilisha vijiji 10 Kila Mwezi na ifikapo Julai 2024 vijiji vyote 75 vitakuwa vimefikiwa.
Pia aliwashukuru na kuwapongeza Mhe Mbunge wa Jimbo la Ngara Kwa ufuatiliaji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan .
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa