- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakuasanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wamehimizwa kuacha tabia ya kukusanya fedha ya serikali kwa kutumia vitabu, badala yake waikusanye kwa kutmia kifaa cha kukusanyia mapato kinachojulikana kama ‘Point of sale’ (POS).
Wito huo umetolewa June 19, 2018 na Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu William Kamanzi, wakati wa semina ya siku mbili ya kuwafundisha wakusanya mapato hao jinsi ya kutumia mashine hizo za POS.
Ndugu Kamazi amesema kwamba, Halmashauri imenunua mashine za POS kwa awamu mbili tofauti, ambapo kwa sasa inazo mashine zipatazo 65 za kukusanya mapato.
Amefafanua kwamba katika awamu ya pili Halmashauri imetumia zaidi ya shilingi milioni 20.6, kununua mashine 35, ambazo zimegawiwa kwa wahusika 30, ambao wamepewa mafunzo ya siku mbili yaliyohusu jinsi ya kutumia mashine za POS.
Ndugu Kamanzi amewataadharisha watumiaji wa mashine hizo, kwamba watatakiwa kurejesha fedha ya serikali baada ya kuikusanywa, ili iweze kupelekwa benki, na kwamba pale mashine zitakapokuwa na tatizo waliripoti mara moja kwa wataalamu.
Aidha, amewataka kutunza neno la siri, na kwamba wanatakiwa kutunza mashine hizo na fedha, iliyokusanywa ambayo haijakabidhiwa ofisini.
Wakusanya mapato nao wameishukuru Halmashauri kwa kuwapa mafunzo hayo, ambayo wamedai yatakuwa na manufaa, na kwamba yatawarahisishia ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku mbili tangu Juni 18-19, 2018, na kuwahusisha wakusanya mapato ya Halmashauri wapatao 30, na maafisa TEHAMA wawili.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa