- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baadhi ya Wazazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuacha tabia ya kuwashawishi watoto kwa makusudi kufanya vibaya mithani yao ya kuhitimu masomo, wakati watoto hao wanauwezo wa kufanya vizuri.
Akisoma risala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara wakati wa kuhitimisha Wiki ya Elimu Mei 30, 2018, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kanazi Ndugu Yusuph Jawabu, amesema kwamba wazazi hao, wanakwamisha juhudu za kuinua taaluma katika Halmashauri hiyo.
“Elimu ndiyo nguzo itakayotuwezesha kumudu maisha yetu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia, tunapoendelea kuujenga uchumi wa viwanda hapa nchini, hivyo kuwaelekeza watoto kufanya vibaya katika mitihani kunakinzana na dhamira ya serikali.” Alisema ndugu Jawabu.
Kwa msistizo alisema kwamba tabia hiyo haikubaliki, kwani atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria, na kuongeza kuwa serikali inatoa elimu bila malipo, ili watoto wote wapate elimu na si kinyumeche.
Ameushukuru uongozi wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa kuweka bayana jitihada zinazofanywa na serikali, katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini ikiwemo; ujenzi wa miundo mbinu ya shule kama vile maabara, madarasa, nyumba za walimu na rusuku ya kuendesha shule hizo.
Siku ya kilele cha Wiki ya Elimu katika Halmashauri ya Wialaya ya Ngara imehitishwa Mei 30, 2018, na kuwajumuisha wakuu wa idara na vitengo mbalimbali, wakuu wa shule, walimu, wanafunzi wa sekondari na wa msingi, pamoja na wananchi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa