- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wamepokea kwa bashasha miradi ya kilimo na ufugaji, itakayofadhiliwa na mradi wa Local Areas Development Projects (LADP), katika eneo lanaloathirika na mradi wa Regional Rusumo Falls Hydroelecric Projects (RRFHP).
Wakiongea na wahamasishaji wa mradi huo Juni 18, 2018, kutoka ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara; wananchi hao wamesema wanakubali na wanaupokea mradi huo, na wako tayari kutoa ushirikiano pale watakapohitajika kufanya hivyo.
Wananchi hao wameomba mradi huo utakapoiva wapewe mbegu za kutosha na kwa wakati mwafaka ili waweze kufanyakazi kwa muda mwafaka kwa lengo la kujiinua kiuchumi.
Mh. Diwani wa Kata ya Mbuba Ndugu David Ilafasha Buzutu, amewataka wananchi waliohudhuria kikao hicho, kupeleka taarifa hizo kwa wananchi ambao hawakupta fursa ya kuhudhuria ili yale waliyojifunza yaweze kuwasafakia.
Amewataka vijana kujiunga katika vikundi, ili waweze kutumia fursa hiyo, kujikwamua kiuchumi badala ya kushinda vijiweni, ambako amedai kwamba hakuna tija.
Mradi wa LADP utafanyakazi na vijiji 22 vilivyomo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa upande wa Tanzania, nchini Burundi utananyakazi katika mikoa ya Busini na Giteranyi ambapo nchini Rwanda upo katika Wilaya za Ngoma na Kirehe.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa