- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wamewatakiwa kulipa kodi kwa kudai risti pindi wanunuapo bidhaa, ili serikali ipata fedha ya kutoa huduma iliyotukuka kwa wananchi hao.
Rai hiyo aliitoa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti Agosti 03, 2018, kwa Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Ngara, kwamba kama wananchi hawatatimiza wajibu wao kwa kulipa kodi huduma haitapatikana.
“Nitoe rai ya kuripa kodi, ninafahamu wilaya ina vituo viwili vilivyopewa milioni 400 kila kimoja, serikali inajenga meli mpya na kukarabati mbili za zamani, zenye thamani ya shilingi bilioni 152, fedha zote zinatokana na kodi ya wananchi.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Ili kufanikisha azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo; TRA katika mkoa huu, wakusanye mapato ya serikali kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanatumia mashine, ili waweze kulipa kodi kadiri wanavyouza.
Amewataka viongozi na watumishi wote kuwa msatari wa mbele kudai risti wanaponunua bidhaa, ili kodi inayokusanywa iweze kuisaidia serikali kutoa huduma iliyotukuka kwa wananchi wake.
Haikubaliki wananchi wadai huduma wanazohitaji katika hospitali, barabara, shuleni, na watumishi wadai kuongezwe mishahara kwa asilimia 100, wakati wanaponunua bidhaa wanaacha fedha ya serikali kwa kutodai risti.
Akitoa mfano, aliwataka viongozi kuwashawishi wananchi wadai risti, ili kodi ya serikali iende katika mlolongo ulio sahihi, na hatimaye wananchi waweze kupata maendeleo kupitia mkondo unaoeleweka na ulio sahihi.
“Mimi binafsi ni muumini mzuri wa kudai risti, ninawaomba wananchi wenzangu mliopo hapa tuwe na msukumo katika suala la kudai risti, ili tuwasukume wafanyabiashara watoe risti; tunapoteza mapato ya serikali kizembe, kwa kweli haikubaliki.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Wwakati huo huo, wafanyabiashara walimuomba Mkuu Mkoa kuwasaidia katika masuala ya malipo ya kodi, kwa madai kwamba TRA wanawanyanyasa kwa kuwatoza kodi nyingi, ambazo zinawakwamisha katika shughuli zao.
Brigedia Jenerali Gaguti amewaahidi kwamba akimaliza ziara yake mkoani Kagera atakutana na uongozi wa TRA mkoa, ili waweke mikakati mahsusi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Amesema yeye pamoja na uongozi wa TRA kutoka kila wilaya katika Mkoa wa Kagera, watatafuta mbenu za kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara; huku wakiwaondolea vikwazo visivyokuwa vya lazima katika kulipa kodi ya serikali.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa