- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara Leo 22/04/2024.
Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano halmashauri ya wilaya ya Ngara imeendelea na sherehe za maadhimisho hayo kwa kufanya shughuli za kimaendeleo kama upandaji wa miti. Miti 36,000 ilikishapandwa kwenye maeneo mbali mbali ya shule za msingi, sekondari pamoja na maeneo binafsi ambapo shughuli hizo za upandaji miti ziliendeshwa na TFS.
Kwenye mwendelezo wa maadhimisho miaka 60 ya muungano halmashauri ya wilaya ya Ngara utafanyika usafi wa mazingira ambao utasimamiwa na mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara Pamoja na viongozi wote.
Lakini pia mkuu wa wilaya Mhe. Col Mathias Julius Kahabi ataongoza shughuli ya upandaji miti katika shule ya Ngara High School siku ya jumanne tarehe 23/04/2024
Hitimisho la Maadhimisho ya miaka 60 ya muungano litafanyika siku ya alhamisi katika uwanja wa posta ya zamani ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col col Mathias Julius Kahabi. Aidha michezo mbalimbali ya ngoma za za asili na kimira pamoja na maonyesho ya vyakula vya asili yataendelea katika tamasha hilo.
Baada ya maadhimisho hayo kutakuwepo na hotuba ya mhe rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan saa tatu usiku katika viwanja vya ya zamani. Na baada ya hotuba tamasha litaendelea mpaka saa sita usiku likisindikizwa na burudani kutoka kwa Wasanii wa nyumbani.
Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Ngara Mhe. Solomon kimilike
Nembo mpya ya miaka 60 ya muungano
afisa utamaduni halmashauri ya wilaya ya Ngara akisaini kitabu maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu wa idara ya Utumishi na utawala akisaini kitabu, ikiwa ni kuungana na Watanzania wote kuadhimisha miaka 60 ya muungano.
Katibu TALGWU Ngara akisaini kitabu maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kauli mbiu ni miaka 60 ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania "tumeshikamana na tumeimarika, kwa maendeleo ya Taifa letu".
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa