- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Yamefanyika Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.
Wilaya ya Ngara ilianza Maadhimisho tangu tarehe 4/12 Hadi 9/12/2023 Kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kupamba Ofisi za Serikali, kuwepo Kwa vitabu vya kusaini, uhamasishaji kupitia vyombo vya habari , kuongea na wazee maarufu/watumishi wastaafu,kufanyika Kwa zoezi kabambe la Usafi,upandaji wa miti 7008,Matembezi ya kilometa 8, kufanyika Kwa mazoezi ya pamoja, michezo Mbalimbali, kufanya kongamano/ Mdahalo,pamoja na zoezi la Uchangiaji Damu.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe.kanali Mahias Julius Kahabi.pia Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike, Mwakilishi wa Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara , Mwakilishi wa Mhe Mbunge Jimbo la Ngara Ndaisaba G Ruhoro, katibu wa chama Cha Mapinduzi Bi Anastazia Amas.
Aidha Viongozi Mbalimbali wa chama na serikali, wananchi walioshiriki Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa