- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiwilaya zilianza Tarehe 17/04-26/04/2023 .Kwa kufanya shughuli Mbalimbali.
Shughuli zilizofanyika ikiwa ni kupamba Ofisi za Serikali Kwa Bendera ya Taifa, na kuwekwa picha za viongozi waasisi wa Muungano ,picha ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na vitabu vya kusaini viongozi ,Wananchi Ofisi za Mhe Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya .
Katika Maadhimisho hayo lilifanyika zoezi la upandaji miti ambapo viongozi walipanda miti 25 Maeneo ya ofisi za Mhe Mkuu wa Wilaya ,Halmashauri , uhamiaji na Magereza Ngara mjini.Aidha miti 268 imepandwa na wananchi.
Zoezi la usafi wa Mazingira lilifanyika Kwa viongozi na wananchi kufanya usafi maeneo ya Sokoni ,Stendi Ngara Mjini na Nakatunga ambapo walijitokeza viongozi wa Serikali,Taasisi,wafugaji,wafanyabiashara wananchi kujumuika na Mhe Mkuu wa Wilaya Ngara Kanali Mathias Kahabi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Constantine Msemwa, Kaimu katibu Tawala Ndg Jawadu Yusuph kufanya usafi.
Zoezi la uandishi wa Insha lilifanyika Kwa Shule za Msingi na Shule za Sekondari,na kuwasilishwa mkoani
Aidha yalifanyika Mahojiano maalum MUUNGANO wetu kupitia Radio kwizera na kaimu katibu Tawala Wilaya alishiriki,pia Wazee maarufu walishirikishwa na kurekodiwa kupitia Halmashauri .
Siku ya kilele tarehe 26/04/2023 yalifanyika matembezi ya km 6.5 kuanzia uwanja wa Posta ya zamani Hadi Buhororo na kurudi ambapo matembezi yalipokelewa na Mgeni Rasmi kaimu Katibu Tawala wilaya aliyemwakilisha Mhe Mkuu wa Wilaya .
Ilitembekewa miradi 9 yenye thamani ya Tsh 1,184,909,428.8 ambapo zoezi lililoongozwa na Mhe Mkuu wa Wilaya Kanali Mathias kahabi na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon kimilike miradi hiyo ni Vyumba 5 vya Madarasa Rulenge, Hospitali ya Wilaya jengo la mama na mtoto,Nyumba ya Mtumishi Mkurugenzi Mtendaji,Matengenezo ya Barabara km 1.1 Murugalama mabawe, Matengenezo makalvati ya zege km 2 Kabanga -kasange,Matengenezo ya sehemu korofi km 4 changalawe na makalvati, na ujenzi wa Daraja katika Barabara ya kilinzi- Mursagamba ,Mtakuja -Rulenge Sokoni
Yalifanyika mazoezi ya viungo Aerobic na michezo mbalimbali ya Kuvuta kamba watumishi serikali vs watumishi NMB, soka wanawake Ngara Queen vs Moonshine ,Soka wanaume watumishi Serikali vs Viongozi wa madhehebu ya Dini zawadi zilitolewa Kwa washindi wa Soka.
Shughuli za michezo zikiendelea lilifanyika zoezi la uchangiaji Damu salama wananchi 85 walijitokeza kuchangia benki ya Damu salama ambapo jumla ya unit 83 zilipatikana.Upimaji Magonjwa mbalimbali ambapo wananchi 189 walipima Magonjwa ya shinikizo la Damu,kisuari na UKIMWI.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa