- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maadhimisho ya siku ya sheria yamefanyika viwanja vya mahakama ya Wilaya iliyopo Ngara Mjini.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya Mhe Col Mathias J. Kahabi aliyewakilishwa na Ndg. Jawadu Yusuph Afisa Tarafa Nyamiaga. Sherehe zilihudhuliwa na waheshimiwa Mahakimu wote, Wana Sheria wa Serikali na wakujitegemea , kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Wakuu wa Uhamiaji ,Takukuru, Polisi, Usalama, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Ustawi wa Jamii ,Viongozi wa madhehebu ya Dini wazee Mzee kidyamasaka , Mzee obed Nkwale viongozi wa Chama na serikali pamoja na Wananchi.
Ilielezwa kuwa maadhimisho Rasmi yalizinduliwa kitaifa tarehe 24/01/2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo maadhimisho kiwilaya yalizinduliwa tarehe 28/01/2024 Kwa kufanya mazoezi ya pamoja, kutembea Kilometa 3, na Mchezo Kufukuza kuku katika uwanja wa Posta ya Zamani Ngara Mjini.
Kauli Mbiu Ikiwa "UMUHIMU WA DHANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA:NAFASI YA MAHAKAMA NA WADAU KATIKA KUBORESHA MFUMO JUMUISHI WA HAKI JINAI".
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa