- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maadhimisho yamefanyika kijiji cha Nyamahwa Kata ya Nyakisasa Wilayani Ngara Mkoa wa kagera.
Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Julias Kahabi ambaye aliiambatana na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya , kamati ya usalama Wilaya , Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri na viongozi wengine wa Chama na serikali.
Taarifa fupi ya maadhimisho iliwasilishwa na Mratibu wa UKIMWI Wilaya Bi Josephina Lusatira katika eneo la tukio.
Shughuli zilizofanyika katika maadhimisho hayo kijiji cha Nyamahwa ni ushauri Nasaha na upimaji VVU Kwa hiari, Tohara Kwa Wanaume,Uzinduzi wa klabu shule ya Msingi Nyamahwa ya kupinga UKIMWI na Mimba katika umri Mdogo pamoja na zoezi la kupanda miti ya matunda aina ya Miparachichi ya kisasa .
Aidha Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Kahabi alisaini hati ambayo ilikabidhiwa .
Maadhimisho hayo pia yamefanyika kijiji cha Bugarama Kata Bugarama Wilayani Ngara Kwa kupima VVU Kwa hiari na kuchangia Damu salama chini ya kampuni ya Tembo Nickel .
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Julius Kahabi aliwashukuru Kwa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani pia vikundi vilivyotumbuiza katika maadhimisho vilitoa ujumbe ulioendana na siku hiyo.
Baada ya maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Kahabi alifanya mkutano wa Hadhara kusikiliza na kutatua kero Kwa wananchi.
Wananchi wasema kero zao ambazo ziligusa sekta za Afya, Maji, Barabara ,kilimo na Mifugo, na Masuala ya uwezesheaji mikopo Kwa vijana.
Mratibu wa UKIMWI Wilaya Josephina Lusatira akifaya zoezi la utambulisho katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya Mhe Mathias Julius Kahabi akipanda Mti Ikiwa ni kumbukumbu ya maadhimisho kiwilaya kijiji cha Nyamahwa Kata ya Nyakisasa.
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa UKIMWI Bi Josephina Lusatira Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ,viongozi Afisa tarafa Rulenge na wanafunzi baada ya zoezi la upandaji Miti.
Mkuu wa wilaya Ngara Mhe Kanali Mathias Julius kahabi akisaini kitabu.
Kikundi Cha sanaaa Cha shule ya Msingi Nyamahwa wakitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi.
Wananchi waliojitokeza katika maadhimisho kiwilaya kijiji cha Nyamahwa Kata ya Nyakisasa.
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mathias Kahabi akiongea na wauguzi wapimaji VVU Kwa hiari.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya Ngara Mhe.Kanali Matias Julius Kahabi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa