- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera, leo tarehe 01 Desemba umeungana na Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani, ki Mkoa Wilayani Ngara katika viwanja vya Posta Ya zamani Ngara Mjini ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila.
Katika maadhimisho hayo, Mhe. Chalamila amekagua mabanda mbalimbali ya wadau na mashirika yanayojishughulisha na huduma za afya hususani yanayopambana dhidi ya maambukizi ya UKIMWI. Ambayo ni MDH, PACT, TADEP, HUMULIZA na AMREF.
Katika hotuba yake kwa wananchi, Mhe. Chalamila ameeleza kuwa kundi linaloongoza kuwa na maambukizi mapya ni kundi la vijana wenye umri wa kati ya miaka15 hadi 24 hali ambayo ni tishio kwa nguvu kazi na Israël wa Taifa letu.
“Katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, Mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliopo tumedhamiria kwa pamoja kupambana na tatizo hili hadi kufanikisha kutokomeza kabisa katika Mkoa wetu. Kwa upimaji uliofanyika kwa kipindi cha mwaka 2022 kuanzia mwezi Januari-Novemba 15,2022, kiwango cha maambukizi mapya kimepungua hadi kufikia asilimia 2,” ameeleza RC Chalamila.
Aidha, katika kufikia malengo ya mkakati wa 95, 95, 95 (tisini na tano tatu) mpaka kufikia mwezi Septemba, 2022 asilimia 97.85 ya lengo la asilimia 95 ya watu wanaokadiriwa kuishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI walikuwa wamefikiwa na asilimia 97.3 ya walioanza kutumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI walikuwa na virusi vilivyofubaa.
Sambamba na hayo ameeleza juu ya changamoto mbalimbali katika kufikia asilimia 95 ya kwanza ya kimamkati, kwa upande wa wanaume kutokujitokeza katika upimaji ukilinganisha na wanawake, maeneo mengi kutofikika kwa huduma zote za afya hasa upimaji, kutokutaja kwa mshirika wa ngono ili aweze kupimwa na unyanyapaa. Serikali imeendelea kupambana na changamoto hizo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Amewaomba wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kuwa na tabia ya kupima afya kila mara na kusisitiza Kamati zote za UKIMWI katika ngazi zote Zifanye kazi, takwimu ziandaliwe na kuwekwa wazi kwa kila eneo na elimu ya kujikinga na maambukizi iendelee kutolewa zaidi kupitia vyombo vya habari vilivyopo Mkoani Kagera.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa