- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Akieleza Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilayani Ngara Ndg Emmanuely Kulwa ,kuwa walikwishaanza maadhimisho Kwa siku kumi na sita 16 za kufanya Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Maadhimisho hayo yamefanyika shule ya Msingi Ngara Mjini ambapo wanafunzi wote wamepatiwa mafunzo ya kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto pia walimu wameshiriki.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii alisema shughuli zilizofanyika katika shule ya Msingi Ngara Mjini ilikuwa ni Kutoa mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia , kubainisha vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ndani na nje ya shule na Uundaji wa dawati la ulinzi na usalama wa Mtoto .
Nae Afisa Elimu Msingi Wilaya Bi Josline Bandiko aliwashukuru Idara ya Maendeleo ya Jamii Kwa Kwa Kampeni hiyo kuifanyia shule ya Msingi Ngara Mjini pia alipongeza Kwa kuanzishwa Dawati la ulinzi na usalama wa Mtoto shuleni.
Wanafunzi wakisikiliza wawezeshaji.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa