- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Chama cha Ushirika cha Wakulima, Ngara Farmers kimeahidi kulipa madeni yote ya wakulima wa kahawa wilayani Ngara mpka inapofikia Novemba 17 mwaka huu. Akijibu maswali ya Waheshimiwa Madiwani katika kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 06 Novemba 2019 katika ukumbi wa Halmashauri Ngara,Mwenyekiti wa chama hicho cha Ushirika Ndugu David Bukozo alisema kuwa malipo ya kahawa wilayani Ngara yamecheleweshwa na wakulima wenyewe kwani Serikali ilitoa maelekezo ya kuwalipa wakulima wa kahawa kupitia akaunti zao za benki na wengi wa wakulima walikuwa hawajafungua akaunti benki hivyo kufanya zoezi la ulipaji kuchelewa.
Mwenyekiti wa Ngara Farmers aliongezea kwa kusema kuwa,tayari mwitikio wa wakulima katika kufungua akaunti benki umekuwa mkubwa na hivyo kuwafanya wao kuwalipa wakulima hao kwa muda na wanatumaini mpka kufikia Novemba 17 wakulima wote watakuwa wameingiziwa pesa zao kwenye akaunti zao.
Baada ya mwenyekiti kutoa majibu ya maswali ya madiwani,Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Kan. Michael Mtenjele alielezea faida za wakulima kufungua akaunti za benki ikiwemo kuwahakikishia usalama wa pesa zao pindi wanapolipwa na pia kuwarahisishia kupata mikopo toka benki pindi wanapohitaji fedha kwa ajili ya mbolea na vitendea kazi wakati wa upandaji wa kahawa.
Katika kikao hicho,Mwenyekiti wa kikao ambae ni mwenyekiti wa Halmashauri aliwaomba chama cha ushirika cha Ngara Farmers kuhakikisha wakulima wote wa kahawa wanaodai malipo yao wamelipwa ndani ya muda ambao wameahidi kuwalipa wakulima wote.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa