- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwahamasisha wananchi, ili waweze kushiki kikamilifu katika kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya wilayani humo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dr. Marco Mbata, ameyasema hayo Julai 10, 2018, wakati alipopewa nafasi ya kuongea na wajumbe wa Bodi ya Afya ya Wilaya ya Ngara, kwamba madiwani wanawajibika kuwahamasisha wananchi, washiriki katika miradi hiyo.
“Nadhani waheshimiwa madiwani mko hapa naomba muwahamasishe wananchi; serikali kuleta fedha si kwamba fedha hiyo peke yake inatosha; kwa sababu hata serikali ikitoa zaidi ya milioni 700 kwa mradi mmoja tu badi fedha hiyo haitoshi.” Alisema Dr. Mbata.
Amewataka wajumbe wajitahidi kusimamia shughuli za maendeleo ya Halmashauri; kwa maana ya huduma za jamii; na hasa usimamizi wa ujenzi wa vituo vya afya vinavyofadhiliwa na serikali ya Muungano wa Tanzania.
Amewataka wajumbe kusimamia fedha iliyotolewa na Mh. Rais Joseph Pombe Magufuli kujenga vituo vya afya, ili thamani ya fedha hiyo iweze kuonekana wazi wazi, na kuonya kwamba fedha hiyo hata mtu akiidokoa bado itaonekana tu.
Kwa hiyo amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Afya na wajumbe wake kuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa hakuna ubadhirifu unaojitokeza badala yake, wawe wazi katika kila hatua wanayofikia, huku wakitunza nyaraka zote muhimu.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Wilaya ya Ngara Dr. Abrahamu Katesigile amemhakikishia Mganga Mkuu huyo wa mkoa Dr. Mbata, kwamba Bodi itajitahidi kuyatekeleza hayo; huku akiwataka wajumbe wa Bodi kuwa kitu kimoja hadi miradi ya Afya ya Murusagamba na Mabawe ikamilike.
Amemshukuru Mganga Mkuu huyo kwa ushauri na mawazo aliyowapa, kwani yanalenga kufanikisha lengo la Mh. Rais Pombe Magufuli la kufungua vituo vyote kwa siku moja; huku akidai kwamba bodi yake italisimamia hilo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara Dr. Revocatus Ndyekobora, aliwaambia wajumbe wa bodi kwamba miradi ya ujenzi katika vituo vya afya vya Mabawe na Murusagamba, inaendelea vizuri kwani mafundi wanatandaza nyaya za umeme na mabomba ya maji.
Kikao cha siku moja cha Bodi ya Afya ya Wilaya ya Ngara kimefanyika Julai 10, 2018, katika ukumbi wa Idara ya Kilimo, na kuwajumuisha wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Marco Mbata.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa