- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mh. Erick Emmily Nkilamachumu na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Aidan John Bahama wakati wa kikao cha mkutano wa baraza la madiwani la robo ya kwanza 2017/2018 kilichofanyika tarehe 31 Oktoba 2017.
Akiongea katika mkutano huo wa baraza la madiwani Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri aliwasisitiza madiwani kuhakikisha wanashirikiana na watendaji katika maeneo maeneo yao kuibua vyanzo vipya vya mapato na kusimamia ipasavyo ili kuboresha mapato ya halmashauri.
Aidha alimtaka Mkurugenzi Mtendaji kuwawajibisha watendaji watakaozembea kukusanya mapato katika maeneo yao na kila baraza la kupokea taarifa za kata basi maafisa watendaji wa kata wawepo ili wasikilize hali ya mapato katika kata nyingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji alieleza kuwa halmashauri imeanza mchakato wa kuanza kukusanya ada ya majengo (Property Tax) baada ya chanzo hicho kurudishwa kwenye Halmashauri, hii ni sambamba na kukusanya madeni ya mwaka jana ya chanzo hicho.
Hatimaye wote kwa pamoja waliwataka madiwani wote kuendelea kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kumeza dawa ya vikope na kushiriki kikamilifu katika zoezi la kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani. Msisitizo huo ulikuja kwa kuwa katika wilaya hii bado ugonjwa wa Maralia ni tatizo na katika utafiti uliofanyika ndani ya wilaya asilimia 10 (10%) ya wakazi waligundulika kuwa na ugonjwa wa vikope.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa