- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni afisa elimu wa shule za msingi ndugu Gideon Mwesiga akifungua mafunzo ya mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (Facility Finanial Accounting and Reporting System ''FFARS'') kwa waratibu elimu kata, wakuu wa vituo vya afya na wahasibu wa hospitali. Katika ufunguzi huo Mkurugenzi aliwasihi washiriki wote wa mafunzo haya kuhakikisha wanasikiliza kwa makini ili mafunzo haya yakapate kuwa na tija kwa namna moja au nyingine. Alishukuru watu wa marekani ambao ndio wadhamini wakubwa wa mradi huo kwa kudhamini mradi ili kuwe na uwazi katika utoaji wa taarifa za fedha katika vituo vinavyotoa huduma. Alisisitiza kwamba serikali ya awamu ya tano inataka kuendana na wakati na ndio maana inaanzisha mifumo mipya kila siku kwa ajili ya kuhakikisha shughuli zake za kila siku zinaendana na teknolojia iliyopo. Hivyo watumishi hawana budi kuipokea mifumo hiyo mipya kwani inasaidia kurahisisha majukumu ya kila siku katika Halmashauri hasa kama mifumo hiyo huhusisha masuala ya fedha. Aliwatakia washiriki mafunzo mema ila wahakikishe wanaelewa na kama kuna sehemu mtu atashindwa kuelewa basi asisite kuuliza swali ili aweze kupatiwa ufafanuzi wa kutosha na ili kila mtu atoke ameelewa kwa ajili ya kwenda kuwafundisha wenzao waliopo vituoni kwa ufasaha.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa