- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watendaji wa kata na vijiji wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyohusisha jinsi ya kukusanya mapato kwa njia ya kieletroniki. Mafunzo haya yalianza siku ya Alhamisi ya tarehe 20 na kumalizika siku ya Ijumaa ya tarehe 21. Lengo kubwa ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kila mtendaji wa kata na kijiji ambaye alihudhuria mafunzo hayo ambao ndio wakusanyaji wakuu wa mapato katika ngazi ya halmashauri anaelewa namna ya kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki. Katika kuongeza ufanisi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, halmashauri ya wilaya ya Ngara imeongeza mashine za kielektroniki (POS-Point Of Sell) 30 ili ziweze kusaidia katika zoezi zima la ukusanyaji wa mapato ndani ya wilaya. Hii itasaidia kuendana na maagizo ya serikali ambayo yanazitaka taasisi zake kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ili kuepusha urasimu katika eneo la mapato, kuendana na mabadiliko na matumizi bora ya tehama lakini pia kuwepo na uwazi katika zoezi hili zima.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa