- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Yamefanyika mafunzo ya mfumo wa kielektroniki katika Ukumbi wa ST FRANCIS uliopo Ngara Mjini.
Washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni Wakuu wa shule za Sekondari ,walimu Wakuu wa shule za Msingi,waganga wafawidhi, watendaji wa Kata na watendaji wa Vijiji.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon Kimilike Ili kuwezesha Ununuzi wa UMMA Ngazi ya Jamii kufanyika kupitia mfumo wa NeST.
Akieleza mkuu wa kitengo Cha Ununuzi na ugavi Ndg. Stivine Mhina Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya alisema Hadi kufikia mafunzo haya Halmashauri ilikuwa imetekeleza agizo la Serikali ambapo iliagiza kuwa ifikapo octoba 2023 Halmashauri Zote nchini zinapaswa kutumia katika Ununuzi wa vifaa,huduma,na kandarasi kupitia mfumo wa NeST ,Halmashauri ilitekeleza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mwl Enock Ntakisigaye.
Washiriki wa mafunzo ya mfumo wa NeST wakiwa kwenye Ukumbi wa ST FRANCIS Ngara Mjini.
Washiriki wa mafunzo walimu Wakuu, Wakuu wa shule, waganga, wafawidhi, watendaji wa Kata na vijiji.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa