- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Ndg Gedion S. Mwesiga (Hayupo kwenye picha) wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa mipango na bajeti wa mamlaka ya serikali za mitaa (PLANREP) na mfumo wa usimamizi wa fedha katika vituo vya kutolea huduma (FFARS) aliwashukuru washiriki wa mafunzo hayo kwa kuwa watulivu na wasikivu kwa kipindi chote cha mafunzo.
Aliwataka washiriki kutumia elimu waliyoipata mara mfumo utakapoanza kutumika rasmi kuandalia bajeti, ambapo mategemeo ni kuanza kutumika katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019. Pia amewataka kuwaelekeza wenzao ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo.
kwa upande wa FFARS kaimu mkurugenzi amewataka wakuu wa idara wenye vituo vya kutolea huduma vitakavyotumia mfumo huo, kuweka mazingira wezeshi ili zoezi la kuingiza taarifa za kifedha kwenye mfumo huo liweze kufanikiwa. Amewakumbusha wakuu wa idara hizo (Elimu Msingi, Elimu Sekondari na Afya) kuwa taarifa hizo za kifedha zinapaswa kuwa zimeingizwa kwenye mfumo wa FFARS kabla ya tarehe 30 Oktoba 2017.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 26 - 30 Septemba 2017 yaliendeshwa na wataalam kutoka idara za Mipango, Fedha, Afya na kitengo cha TEHAMA na Uhusiano.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa