- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Afisa Elimu Msingi (aliyevaa suti) ndg. Gideon Samson Mwesiga akipokea madawati 100 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Kabanga Nickel ndg.Boniface P. Shuuli. Madawati hayo ni sehemu ya ahadi ya madawati 120 ambayo yaliahidiwa na kampuni ya Kabanga Nickel kwa Halmashauri ya wilaya ya Ngara katika kutokomeza tatizo la madawati wilayani Ngara ili kutekeleza agizo la raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Dokta John Pombe Joseph Magufuli. Tukio hili lilifanyika katika kata ya Rulenge eneo la Mission. Hata hivyo afisa uhusiano wa Kabanga Nickel alisisitiza suala la halmashauri kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuwezesha miradi inayofadhiliwa na Kabanga Nickel kukamilika kwa wakati na kutoa msisitizo kwa wananchi pia kutoa ushirikiano wa kutosha pale nguvu yao itakapohitajika kwa namna moja au nyingine katika kuleta maendeleo ndani ya halmashauri yetu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa