- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Ngara Mjini (NGUWASA), katika kipindi cha robo ya tatu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 34.7 na kutumia zaidi ya shilingi milioni 35.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Eng. Simoni Ndyamukama, aliyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha robo ya tatu, kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mwishoni mwa Aprili 2018.
Eng. Ndyamukama amesema kufikia tarehe Machi, 2018, Mamlaka imefanikiwa kuwa na wateja 2,639, na kwamba NGUWASA ina lenga kutoa huduma ya maji kila siku, kwa wakazi wa mji wa Ngara kwa kutumia teknolojia ya mitambo 3 ya kusukuma maji.
“Katika kipindi cha Januari hadi kufikia Machi 2018, hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya mji wa Ngara, ambayo ni Mubinyange, Nyamiaga, Murgwanza, Nakatunga na Buhororo, ilikuwa ni ya wastani.” Alisema Eng. Ndyamukama.
Jumla ya matumizi katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018 mamlaka imetumia shilingi. 35, 794,980, ambapo shilinigi 24, 300,000 zimetumika kulipia gharama za umeme wa kuendeshea mitambo.
Eng. Ndyamukama amesema kwamba, Mamlaka ya Maji imetumia jumla ya shilingi 11, 494,980, kuwalipa wafanyakazi mishahara, kukarabati miundombinu na uendeshaji wa ofisi.
Aidha, amesema hadi Machi, 2018, Mamlaka inadai shilingi 22, 972,820.00, ambapo wadaiwa wakubwa ni taasisi za serikali ambazo ni Magereza inayodaiwa shilingi 18, 180,650, na taasisi nyinginezo zanadaiwa shilingi 2, 831,720.00, ambapo watumiaji wengine wanadaiwa shilingi 1, 960,500.00.
Kupanda kwa gharama za umeme wa kuendeshea mitambo ya kusukuma maji ni changamoto, inayosababisha Mamlaka ishindwe kutekeleza majukumu yake mengine, kwani kwa mwezi mmoja pekee gharama za ankra za umeme zinafikia wastani wa shilingi 12, 000,000.00.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa