- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mashindano yamefanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Rulenge Ngara Kwa kushirikisha Wasanii 23 kutoka katika kata Mbalimbali za Wilaya ya Ngara na Washiriki 2 kutoka Halmashauri ya Biharamulo na kufanya jumla ya washiriki 25.
Aidha mashindano hayo ya kusaka Vipaji vya Wasanii yaliyoandaliwa na MC Oswald Kwa kushirikiana na ofisi ya Utamaduni sanaa na michezo. pia yamehudhuliwa na Wakuu wa Idara za Halmashauri , Afisa Tarafa na Wananchi kutoka sehemu Mbalimbali za Ngara.
Mgeni Rasmi aliyefungua mashindano hayo ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon O Kimilike.
Mgeni Rasmi Bi Sabra Mwankenja amewataka Wasanii kutumia vibaji vyao katika kuendeleza sanaa ikiwa ni pamoja na kujiinua kiuchumi na isitumike sanaa kufanya mambo maovu
Kauli mbiu ya mashindano ni "Kipaji chako ajira yako"
Mashindano hayo yataendelea awamu ya pili.
Wakuu wa Idara na Vitengo Vya Halmashauri wakiwa katika mashindano hayo.
Majaji wa mashindano hayo wakiongozwa na chief Judge Lucas magale wakisikiliza Kwa Makini wakiwa na fomu maalum za alama.
Mambo yakiwa fire jinsi vijana wanavyoonesha Vipaji vyao.
Msanii baada ya kumaliza akiwa na MC -HD.
Majaji.
Picha ya pamoja viongozi na Wasanii kabla ya kuanza mashindano.
Msanii masharti matatu kutoka nyakiziba Ngara.
Afisa Tarafa Rulenge akiwa katika ukumbi wa Malaika Beach Rulenge.
Wasanii ndani ya ukumbi wa Malaika Beach Rulenge Ngara.
Wananchi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa