- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kiasi cha shilingi milioni 592,519,470.03 zimetumika katika mategenezo ya barabara 32 zenye urefu wa kilomita 86, na ujenzi wa makaravati 20 katika barabara 14 katika kipindi cha Julai 2017/2018.
Hayo ni kwa mujibu wa Mhandisi wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Christopher Masunzu ofisini kwake Julai 31, 2018 kwamba matnegenezo haya yamegawanyika katika makundi matano.
Ameyataja makundi hayo kuwa ni matengenezo ya kawaida (routine maintenance) yaliyogaharimu jumla ya shilingi 66,817,152.90 katika barabara zilizoko kata za Kanazi, Mugoma, Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Rulenge, Kibogora, Keza. Murukurazo pamoja Mabawe.
“Haya ni matengenezo ya kawaida ya barabara (routine maintenance) zenye urefu wa kilomita 66.8 katika kata tajwa hapo juu.” Alisema Mhandisi Masunzu.
Matengenezo ya sehemu korofi (Spot improvement) katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Mbuba, Kibimba na Nyamiaga zilizogharimu shilingi milioni 30,529,897.10.
Matengezo ya muda maalumu (periodic maintenance) yametumia shilingi milioni 150, katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Bukiriro, Murusagamba, pamoja na Ntobeye.
Amesema matengezo mengine yalikuwa ya barabara 3 za lami zenye urefu wa kilomita moja zilizojengwa katika Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara na kughatimu jumla ya shilingi za kitanzania 304,297,239.00.
Katika mwaka huo wa fedha TARURA walifanikiwa kujenga makalavati (Culverts) yapatayo 20 katika barabara 14 katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Kabanga, Kasulo, Bukiriro Murukulazo, Kibimba, Mugoma pamoja na Ntobeye.
Aidha, Mhandisi huyo wa TARURA amesema Makalavati hayo yamegharimu jumla ya shilingi Milioni 40,875,200/=; huku akitoa wito kwa wananchi kuzitunza barabara kwa madai kwamba zinatumia fedha nyingi ambayo ingeweza kufanya kazi nyingine za maendeleo.
Amewaonya wananchi wenye tabia ya kulima kwenye hifadhi ya barabara kuacha tabia hiyo mara moja, kwani wanasababisha kuziba kwa mitaro kunakopelekea kuharibika kwa miundombinu hiyo kwa muda mfupi hasa wakati wa mvua.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa