- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika utiaji saini wa matengenezo ya barabara ya Rusumo-Lusahunga Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo itakayofanyika Benaco Ngara tarehe 18.02.2022.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo inayounganisha nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi Dkt.Samia Suluhu Hassan ameona ni muda muafaka wa kufungua uchumi wa Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla kwa kupunguza vikwazo vya barabara chakavu.
"Rais Dkt. Samia Suluhu ameruhusu na kuidhinisha fedha za ukarabati na kujenga upya barabara ya Lusahunga- Rusumo km 92 chini ya mpango wa ushirikiano wa usafiri Tanzania, katika hafla hii tunategemea Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuwa Mgeni Rasmi", ameeleza Mhe. Chalamila
Sambamba na hilo, amesisitiza kuwa pamoja na utiaji wa saini wa mkataba huo, ipo miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani Kagera ambayo ipo katika hatua za manunuzi na kutafuta wakandarasi ikiwa ni pamoja na Omugakorongo kuelekea Kigarama mpaka Murongo, Bugene kuelekea Kaisho mpaka Morongo, Kagera Sugar Junction (Bunazi) kuelekea Kitengule.
Amewasisitiza wananchii pamoja na wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia hafla hiyo ya utiaji wa saini wa mkataba huo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa