- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kikao hicho Mhe. Mbunge aliwapongeza Maafisa hao kwa kazi nzuri ya kuhudumia wananchi wanayoifanya,
Aidha aliwasihi kutilia mkazo zao la Kahawa ambalo katika Mkoa wa Kagera, Ngara imekua mmoja wa wazalishaji wadogo, kati ya tani 49,000 za kahawa ya maganda zilizoripotiwa na Bodi ya Kahawa Kagera msimu wa 2023/2024 kwa mwezi Septemba ni tani 1300 pekee zinazotokea Ngara.
Mhe. Mbunge tangu alipoingia Bungeni 2020, alipambana sana kuona soko la Kahawa Ngara linakuwa bora zaidi, ambapo msimu wa kahawa 2022/2023 lilianzishwa soko la mnada kwa njia ya mtandao lililowezesha bei ya kahawa ya Robusta kupanda kutoka wastani wa 1200 hadi kufikia 2400 kwa kilo Moja ya kahawa ya maganda jambo ambalo halijawahi kufikirika kwa miaka yote tangu kuanza kwa kilimo cha Kahawa katika Mkoa wa Kagera
Leo hii bei ya Kahawa Ngara inafanana na Maeneo mengi Nchini, na kwa sababu hiyo Mhe. Mbunge alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kuitazama Ngara kama eneo muhimu kwa zao la kahawa na kumuomba motisha ya miche ya Kahawa ili kuchochea Kilimo cha zao hilo
Mhe. Rais alitoa kiasi cha TZS 300,000,000 kupitia Bodi ya kahawa ili kuzalisha miche takribani Milioni Moja mahsusi kwa Jimbo la Ngara.
Katika Kikao hicho Mhe. Mbunge aliambatana na Ndg. Annastazia Amos Amas, Katibu wa CCM - Wilaya ya Ngara na Mwakilishi wa Bodi ya Kahawa Kanda ya Ziwa Ndg. Edmond Zani.
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa