- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa wilaya ya Ngara Mh. Rafael Gashaza akiongea mbele ya mkutano wa hadhara, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Rais wa Burundi, katika kiwanja cha Posta ya zamani mjini hapa ameeleza kuwepo kwa kero ya maji hapa wilayani inayosababisha usumbufu wa hapa na pale kwa wananchi. Hata hivo Rais Magufuli ameahidi kuishughulikia kero hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha Tshs milioni 13 kwa ajili ya ununuzi wa Mota, hii ni baada ya kumtaka mhandisi wa maji Eng. Godliver Gwambasa kueleza tatizo la maji wilayani Ngara na kubainisha kuwa tatizo kwa sasa ni Mota ya kiasi hicho cha fedha kwa ajili kisima cha tatu ambapo visima vinavyofanya kazi ni viwili. Pia Rais Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi maombi ya Mbunge kwa kumtuma waziri wa maji kuja kujionea hali halisi hasa eneo la mlima Shyunga linalopendekezwa na mbuge kujenga tanki la maji.
Awali mbunge aliwashukuru marais kwa kuichagua Ngara kuwa mwenyeji wa ugeni huu mkubwa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa