- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Menejimenti ya Halmashauri ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Wilaya, wamefuata na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias J. Kahabi katika ziara ya Kutembelea kijiji cha Murukulazo, Kata ya Murukulazo kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi pia wakiwemo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Ndg. Jawadu Yusuph pamoja na Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg Solomon Kimilike aliyewakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Ndg Emmanuel Kulwa pamoja na Wakuu wa idara na vitengo Mbalimbali Halmashauri ya Ngara na Taasisi za Serikali.
Katika mkutano huo wananchi waliuliza maswali, changamoto na KERO mbalimbali na *kujibiwa papo kwa papo na Wakuu wa Idara na Taasisi za Serikali* ambapo maswali changamoto na KERO zilijikita zaidi kwenye huduma mbalimbali za kijamii na miundombinu kama vile; Elimu, Afya, Barabara, Umeme, Maji, Ardhi, Kilimo na Mifugo.
Mhe Mkuu wa wilaya ameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa elimu ili wananchi wazidi kuwapeleka watoto wao shule kwani watoto hao ndiyo kizazi kipya na tegemezi kwa Taifa siku za baadae.
Mhe Mkuu wa wilaya aliwaeleza Wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki vema katika dhana nzima ya Ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto ndogo ndogo za Kiusalama zilizopo katika Kata na Vijiji vilivyopo mpakani ikiwemo Kata ya Murukulazo.
Mhe Mkuu wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwaonya Wananchi wachache wanaokaribisha wahamiaji haramu toka nchi jirani kwa mwanvuli wa kufanya kazi kama vibarua wa kulima mashamba alisema tabia hiyo lazima iachwe mara moja inahatarisha Usalama wa Mwananchi mmoja mmoja na Jamii kwa ujumla.
Pia amewataka Viongozi wa Kijiji cha Murukulazo kuwa na utaratibu ulipo kwa Mujibu wa taratibu na Sheria wa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi kupitia Mkutano Mkuu wa Serikali ya Kijiji ambapo Wananchi wanaipata fursa ya kuuliza maswali na hoja mbalimbali kuhusiana na taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya kijiji toka vyanzo mbalimbali vya mapato ama toka Serikali kuu, michango ya Wananchi nk.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuleta fedha za Miradi ya Maendeleo Wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa