- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola, ameridhishwa na kazi inayofanywa na kamati ya ulinzi na usalama katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, na kuitaka kamati hiyo kuendelea na kazi; wakati serikali inatafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili.
Mh. Lugola ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja Wilayani Ngara Januari 2019; wakati akiongea na wananchi katika viwanja vya posta ya zamani kwamba Ngara ina amani na utulivu si kama ilivyokuwa mikaka iliyopita.
“Hali ya Ulinzi na salama imeimarishwa katika Wilaya ya Ngara, ikilinganishwa na miaka iliyopita, hii inaonyesha kwamba kazi kubwa imefanyika kuifikisha Ngara hapa ilipo; kwa hiyo, kamati hiyo inastahili pongezi.” Alisema Mh. Lugola.
Amesema serikali itaendelea kudhibiti uarifu, ili wananchi waendelee kufanya shughulizao za kuinua uchumi kwa sababu hapa nchini kuna amani, usalama na utulivuna kuongeza kwamba serikali hivi sasa imeimarisha ulinzi kwa kuweka kambi katika barabara ya Karagwe – Ngara.
Ameisifu kamati ya ulinzi na usalama wilayani Ngara kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo ambazo amezitaja kuwa ni ukosefu wa sare za kutosha, nyumba za askari pamoja mishahara midogo lakini bado wanaendelea kulitumikia taifa hili.
“Kuna baadhi ya askari wasio waadilifu wanaochafua na kuaribu sifa nzuri za vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufanya mambo ambayo hawakutumwa kuyafanya na vyombo hivi; hao dawa yao iko jikoani.” Alisema Waziri Lugola.
Akijibu swali la msongamano gerezani, Mh. Lugola ameitaka ofisi ya mkuu wa polisi Wilaya (OCD) kuzifanya upelelezi wa kesi kwa muda mfupi, ili isaidie kuzuia msongamano wa wafungwa gerezani.
Pia amependekeza wahamiaji haramu badala ya kuwafungwa katika magereza hapa nchini bora wapewe adhabu zitakazowawezesha kurejea nchini kwao badala ya kuwafunga hapa nchini na kusababisha msongamano.
“Kuwafunga hawa wahamiaji haramu kunaongeza msongamano katika gereza zetu; huku tukiendelea kuwatunza kwa gharama za serikali, hivyo nashauri badala ya kuwafunga wapewe adhabu mbadala na warejeshwe makwao.” Alishauri Mh. Lugola.
Kuhusu changamoto zinazovikabili vyombo vya ulinzi na usalama; amesema serikali inafahamu matatizo yanayovikabiri vyombo hivyo, kwa hiyo; amevitaka kuendelea kufanyakazi kwa kujituma, wakati seikali inashughulikia matatizo hayo.
Aidha, ameshauri Halmashauri hapa nchini pale inapowezekana kutumia ‘Own Source’ kusaidia kukarabati baadhi ya miundombinu katika vituo vya polisi, magereza na hata uhamiaji kama wanavyofanya katika shule na vituo vya afya hapa nchini.
Aidha, amewataka askari wote nchini kufanyakazi kwa uadilifu, nidhamu na kujituma huku wakiepuka vishawishi vinavyoweza kuwaingiza katika hatari ya kupoteza kazi na hata kufungwa jera; huku akiwaahidi kwamba serikali itawalinda.
“Mimi nitamlinda askali yeyote anayefanya kazi kwa uhuru, uamakini na kwa nidhamu; lakini sitamlinda askali anayekiuka maadili ya kazi yake; hivyo zingatiani sheria, taratibu na kanuni zinazotawala vyombo vilivyowaajiri.” Alisema Mh. Lugola.
Amewasisitiza askali wote nchini kufanyakazi kwa bidiii lakini zaidi sana kwa ‘team work’ kwa madai kwamba watu wanaofanyakazi kwa upendo na kwa pamoja wanafanikiwa kwani umoja ni nguvu na utengano ni udahifu.
Amesema lengo la ziara yake ni kufahamiana na watendaji kazi wake; lakini zaidi, ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kama inavyoonekana Ibala 04 kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kudumisha umoja, amani, ulinzi na usalama.
Pamoja naye aliambatana na Mkuu wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera (RPC), Mkuu wa Idara ya Vitambulisho vya Taifa, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa, pamoja na mkuu wa jeshi la polisi Mkoa; ambapo baada ya ziara yake Wilayani Ngara, ameendelea na ziara yake Wilayani Biharamulo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa