- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Watendaji na wazazi hamuruhusiwi kusuluhisha migogoro ya wanafunzi waliopata mimba; kwani ni ya kisheria zaidi; badala yake muiripoti katika vyombo vya sheria.” Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele alionya.
Mkuu wa wilaya Lt. Col. Mntenjele ametoa onyo hilo, wakati wa kufunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya, kilichofanyika Machi 02, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya.
Amesema baadhi ya viongozi na wazazi wanasuluhisha migogoro ya wanafunzi waliopata mimba, bila kufuata taratibu za kisheria, hatimaye mtoto wa kike hanufaiki na suluhu hiyo.
“Inapojulikana kwamba mtu amempa mwanafunzi mimba, wazazi wa pande mbili bila kujali maisha ya baadae ya mwanafunizi huyo, lakini wanasuluhisha mgogoro huo kwa faida yao binafsi: tabia hii haikubaliki.” Alisema mkuu huyo wa wilaya.
Amesema, hivi karibuni amechukua hatua za kisheria dhidi ya mtu mmoja, aliyewabebesha mimba wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya Shunga; hatua aliyochukua baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wasamaria wema.
Ametoa rai kwa viongozi na wananchi wilayani Ngara, kutoa taarifa wanapoona matukio ya kuwapatia mimba wanafunzi, ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha, akihojiwa na Radio Kwizera hivi karibuni Afisaelimu wa Mkoa wa Kagera ndugu Aloyse Kamamba amesema kuwa kati ya Wilaya nane za mkoa wa Kagera; Wilaya ya Ngara inaoongoza kwa kuwa na wanafunzi wapatao 60 tangu 2010 hadi 2017, waliosimamishwa masomo kwa sababu ya kupata mimba.
Ndugu Kamamba amewaasa wanafunzi wa kike kujenga tabia ya uvumilivu, kwani kila kitu kina wakati wake, na kuongeza kwamba kamwe masomo hayachanganywi na mapenzi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa