- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe kanali Mathias Julius Kahabi, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon Kimilike pamoja na Kamati ya Uliinzi na Usalama Wilaya ya Ngara ambapo amekutana na Mkandarasi ambae amekua na kasi ndogo sana ya ujenzi Mradi wa Soko la kimkakati lilipo Kahaza - Rusumo Ngara.
Mhe Mkuu wa Wilaya amemtaka Mkandarasi kueleza changamoto inayomfanya asiende Kasi kukamilisha Mradi, Katika hatua ya awali. Ambapo Mkandarasi huyo aliwekwa ndani na aliomba kutolewa Ili kufikia malengo yanayoendana na pesa aliyopewa Taslim Tsh. Millioni 377 ambapo ilipaswa awe amefika 60% na Sasa yupo 33%.
Mkandarasi huyo ameonyesha kutokua na vifaa vya kukamilisha Mradi huo wa ujenzi.
Kwani ameshindwa kujieleza na angeomba apewe muda wakujieleza Kwa maandishi.
Mhe Mkuu wa Wilaya amesisitiza kazi hyo kufanyika na asilimia zifikiwe, aongeze vifaa site na kama Kuna changamoto aziwasilishe Jumatatu tar 8 January asbh ili zipatiwe ufumbuzi na kazi iendeleee.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanali Mathias J.kahabi akiwa anaongea na mafundi katika Soko Mkakati linalojengwa la Kahaza wilayani Ngara.
Mafundi Ujenzi wakisikiliza Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias J. Kahabi eneo la Ujenzi wa soko Mkakati Kahaza wilayani Ngara.
Mhe Mkuu wa Wilaya akiwa kwenye kikao na Mkandaras ili kujua Kwa nini kazi inasuasua.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa