- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ambaye ni Mkiti kamati ya fedha ,utawala na Mipango Mhe Wilbard Bambara akiongoza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Enock Ntakisigaye Wajumbe wa Kamati hiyo ambao ni Waheshimiwa Madiwani na wataalam wa Halmashauri na wasimamizi LADP_( Nile Equatorial lake subsidiary Action program).
Mradi huo ambao una thamani ya Tsh Bilion 3.04 upo asilimia 95 na Kwa Sasa Mradi unaweza Kutoa huduma ya maji Kwa wananchi wa Kata ya Rusumo na Kata Jirani.
Kamati hiyo imetembelea kuona idadi ya miundombinu shirikishi kwenye Mradi huo ambapo imeangalia
1.Tanki la kupokelewa maji Kutoka kwenye chanzo.
2.Tanki la kupokelea maji na kupeleka kwenye Tanki la kuchanganyia dawa.
3.Tanki la kuchanganyia maji yenye dawa
4.Tanki la kutwamisha uchafu unaobaki in kwenye mchanganyo.
5.Tanki la kuchujia uchafu na Kutoa maji safi
6. Eneo la kuhifadhi tope la uchafu
7. Chemba za kusafishia uchafu
8.Tanki la kupokea maji safi baada ya kuchujwa
9.Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita 230,000
10.Vituo 16 vya kuchotea maji
11. Mabomba ya chuma ya kusafishia maji
12. Jengo la kufunga pampu za kusukuma maji kwenda Tanki la kuhifadhia.
13. Jengo la utawala na maabara
14. Jengo la kuhifadhi kemikali
15. Jengo la walinzi
16. Jengo la kuishi wafanyakazi
17. Jengo la vyoo vya imma
18. Uzio kuzunguka eneo la maradi kwenye chanzo.
Kamati hiyo imekubali kupokea Mradi huo Mapungufu madogo yaliyobaki yafanyiwe kazi haraka lakini wananchi waanze kupata huduma ya maji.
Viongozi wa Kamati ya fedha utawala na Mipango wakiwa kwenye Mradi mkubwa wa Maji Rusumo.
Mhe Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara akiwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Enock Ntakisigaye pamoja na Mhe Sunday Mukozi.
Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara akiongoza kamati kutembelea Mradi Mkubwa wa maji Rusomo wilayani Ngara.
Kaimu Mratibu wa LADP akiwa Wajumbe wa Kamati iliyofika kukagua Mradi huo.
Mhe Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara akiwa na makamu wake Mhe Adronizi Bulindori pamoja Waheshimiwa Sunday mkozi, Mhe Sudi Mkubila, Mhe Antonia, Mhe mukiza Byamungu na kaimu Mkurugenzi Ndg Enock Ntakisigaye kwenye Mradi wa Maji.
Mhe John Fabian akiwa na kaimu Afisa Mipango Ndg Mwakikuti Bonface,pamoja na Mwanasheria wa Halmashauri wakili Shaffii Abdull.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa