- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Jamani mkulima wa kahawa mwaka 2018 anauza mwenyewe na kama kuna mkulima aliigia mkataba na mfanyabiashara basi makataba huo ni batiri.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama.
Ndugu Bahama aliyasema hayo Julai 31, 2018 kwa wakati tofauti alipokuwa ziarani, kufuatilia wafanyabiashara, wanaonunua mashamba ya kahawa ya wakulima Wilayani humo.
Amewaambia wakulima wasisubutu kuuza au kununua kahawa kinuyume na utaratibu wa serikali, kwani kufanya hivyo kutawatia hatiani na kwamba ndani ya gari lake ana wafanyabiashara wawili waliokiuka agizo hilo anawapeleka polisi.
Amesema wanatakiwa kuwa waaminifu kwa serikali na kwamba wakisikia kuna mtu ananunua kahawa kwa wakulima wamwambie mtendaji, na kama hawakupata msaada wampigie simu Mkurugenz mwenyewe.
Aidha, amewahakikishia kwamba chama cha Ushirika cha Ngara Farmers Cooporative, kitaanza kununua kahawa msimu huu siku ya Jumatatu ya Agosti 06, 2018, na kwamba wameamua kunua kahawa mapema, kwa sababu kahawa ikikaa muda mrefu inapugua thamani yake.
Mkurugenzi huyo amevunja mikataba kati ya wakulima na wafanyabiashara, na akasisitiza kwamba kila aliyemuuzia shamba la kahawa mfanyabiashara; shamba hilo na kahawa yote ni mali ya mkulima.
“Kila mkulima atakayeuza kahawa atapewa fedha yake siku hiyo hiyo, na kwamba wakulima hao wanahiari ya kupitishia fedha yao benki au kupata fedha yao moja kwa moja.” Alisema Ndugu Bahama.
Serikali ina mkono mrefu mtu asje akauza au kununua kahawa akafikiri kwamba hatajua ndiyo maana wale wote waliojihusisha na mpango huo haramu nimewakamata na kahawa walionunua itakuwa mali ya serikali.
Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Mwivuza alimshukuru sana mkurugenzi huyo, na kumuahidi kumpa ushirikiano, ili wakulima wanufaike na jasho lao kwani wamenyonwa muda mrefu.
Ndugu William Wellington alinukuliwa akisema kwamba tangu mwaka 1978, hajwahi kuanika kahawa nyumbani kwake, ingawa ana mashamba makubwa, bali kazi yake ilikuwa ni kuwatunzia matajiri.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa