- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike wanewasilisha cheti na Tuzo ya pongezi Kwa usimamizi wa Ujenzi wa Shule kupitia Mradi wa SEQUIP 2021/2022 Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Tuzo na cheti ambazo zilikabidhiwa Kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Mhe Mohamed Mchengerwa (Mb) Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani.
Tozo zimetolewa Kwa Halmashauri zilizofanya vizuri kitaifa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Aidha pia Mkurugenzi Mtendaji amesema pia Wilaya ya Ngara imepongewa Kwa kufanya vizuri katika mfumo wa NeST.
Aidha Mkurugenzi amewapongeza Mhandisi Saimon Mtuka, Mwl Enock Ntakisigaye Afisa elimu na kamati iliyosinamia Kwa usimamizi madhubuti wa majengo ya Shule ya Sekondari Chief Nsolo.
Mkurugenzi Mtendaji amewashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo Kwa ushirikiano mkubwa Uliopo wilayani Ngara .amewataka kuendelea na ushirikiano na umoja huo tulionao.
Afisa Elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye akisoma maelezo yaliyoandikwa kwenye chiti Cha pongezi kwenye kikao Cha wataalam wa Halmashauri.
Tuzo.
Mkuu wa Idara ya Utawala,utumishi na rasilimali watu Bi Sabra Mwankenja akiwa na Mkuu Wa Idara ya Elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye wakiwa na Tuzo ya pongezi.
Wakuu wa Idara na Vitengo.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa kwenye kikao Cha Kuwasilisha Tuzo na Cheti tuliyopata Wilaya ya Ngara Kwa usimamizi Mzuri wa Miradi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa