- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan serikali ya awamu ya sita imeleta Zaidi ya shilingi Bilioni 31 katika halmashauri ya wilaya ya Ngara katika sekta ya elimu, Afya na utawala.
Akitoa salam za pongezi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufikisha miaka mitatu, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Mhe. Solomon kimilike amemshukuru Rais Samia kwa upendeleo aliouonyesha kwa wananchi wa wilaya ya Ngara ambapo kwa kipindi chake wilaya hiyo imebadilika katika sekta zote.
Amesema kuwa halmashauri hiyo katika kipindi cha miaka mitatu imejenga shule mpya za msingi 7, sekondari 5, vituo vipya vya afya 3, hospitali ya wilaya, nyumba ya mkurugenzi na jengo la Halmashauri jipya ambalo ujenzi wake unaendelea, Vyumba vya madarasa zaidi ya 200 msingi na sekondari pamoja na maabara za sayansi zaidi ya 21.
Ameongeza kuwa wameweza kujenga soko la kimkakati linalojengwa kata ya Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambalo linakwenda kuongeza mapato katika halmashauri ya Ngara lakini kuongeza wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Dkt. Prisca Temba ni Mganga mfawidhi katika kituo cha afya cha Rusumo kilichojengwa mpakani mwa Tanzania na Rwanda amesema kuwa kituo hicho kimeweza kutatua kero ya huduma ya afya iliyokuwa ikiwasumbua wananchi wa maeneo hayo waliolazimika kutembea umbali mrefu kuifata huduma Ngara mjini.
Nao baadhi ya wanafunzi katika shule za Chief Nsolo na Rusumo Sekondari wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyowaboreshea maisha ya shule kwa kuanzisha shule mpya pamoja na kuweka modarasa hali inayowafanya wanafunzi hao kusoma kwa utulivu.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa