- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Miili ya Watoto Sita wa Familia moja walioaga Dunia Mnamo Novemba 14 na 16, imepumzishwa katika Eneo Maalum la maziko Wilayani Biharamulo .
Shughuli iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Abubakari Mwassa.
Marehemu hao Kutoka katika Familia Moja inadaiwa Novemba 13, walishiriki chakula Cha jioni wakiwa watu 11 wakiwemo watu Watatu na Watoto Nane, ambao kati ya hao ni Watoto Sita waliofariki huku Watoto Wawili na Watu wazima Watatu mpaka Sasa hao ni wazima.
Akizungumza wakati wa Kuaga Miili ya Marehemu hao Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema kuwa Serikali Bado inaendelea na Uchunguzi kubaini chanzo na kwamba Watakuja Wataalam wengine Kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kuendelea na Uchunguzi wa jambo hili, hivyo Wananchi wasiamini sana Taarifa zisizo Rasmi kwa kipindi hiki mpaka pale Taarifa itakapotolewa tena
Taarifa za awali za Kitaalamu zinaonesha kuwa Marehemu hao huenda walikula au kunywa Sumu Kutokana na Dalili zilizoonekana kabla ya kufariki ikiwemo kutapika, kizunguzungu na kutokwa Damu. Hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea Ili kubaini sababu nini kimepelekea Vifo hivyo.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa