- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Julius kahabi ameendelea na ziara ya Ukaguzi wa Miradi.
Mhe Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo aliambatana na kamati ya Usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Solomoni Kimilike pamoja Wataalam wa halmashauri.
Mhe Mkuu wa Wilaya na timu hiyo amekagua Miradi wa ujenzi wa Nyumba ya walimu Shule ya Msingi Nyamikono yenye thamani ya Tsh 100,000,000/=, Shule ya Msingi Chamabale Yenye thamani ya Tsh 100,000,000,/= pamoja na Shule ya Sekondari Mpya ya Murubanga kata ya Nyamagoma Tarafa ya Murusagamba kupitia Mradi wa SEQUIP Kwa Mwaka 2022/2023 wenye thamani ya Tsh 584,280,000.28/=
Aidha, Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ngara anatoa shukrani kwa namna ya kipekee pongezi za dhati Kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa kuendelea kutoa fedha za miradi katika wilaya ya Ngara.
Pia anatoa pongezi Kwa Mhe mbunge Jimbo la Ngara ndugu Ndaisaba George Ruhoro, Mkurugenzi mtendaji Ndg. Solomoni Kimilike, M/Kiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilberd Bambara, Waheshimiwa Madiwani kamati ya ulinzi na usalama,Wakuu wa Idara pamoja kamati ya ujenzi Kwa usimamizi mzuri.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ngara akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi baada ya kukagua Ujenzi huo unaendelea vizuri.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias J. Kahabi wa katikati akiwa na viongozi Mbalimbali.
Mhe Mkuu wa Wilaya Kanali Mathias J.Kahabi akikagua Maabara.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias J.Kahabi akiwa amekaa na viongozi Mbalimbali kwenye Madawati.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa