- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Julius Kahabi katika KampeniI yake kabambe ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Ngara .
Leo tarehe 20/11/2023 amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Chivu ,Kigina Kata ya Ntobeye.
Mkuu wa wilaya katika Ziara hiyo alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya, Katibu Tawala Wilaya,kamati ya usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri,Wakuu wa Taasisi za Tanesco,Ruwasa,Tra, Nida,Tarura na kiongozi wa Nelsap.
Lengo la mkutano huo wa hadhara Ikiwa ni kusikiliza na kutatua kero mbalimbali ambazo wananchi (waguswa)wa kijiji cha Chivu ,Kigina akidai fidia kuhusu athari za ufuaji umeme wa Rusumo .
Mkutano huo uliongozwa na Mhe Mkuu wa wilaya Kwa kusikiliza kero na wataalam Kutoka Halmashauri, Taasisi aliyeongozana nao kuzijibu Kwa kuzitatua kero zilizotolewa na wananchi.
Wananchi wamempongeza sana Mhe Mkuu wa wilaya Kwa kuamua kufanya mikutano ya hadhara Kwa kuwafuata wananchi kwenye Kata zao kusikiliza na kutatua kero walizonazo .Aidha wamesema Sasa wameondokana na adha ya kwenda kupeleka kero katika Ofisi za Serikali .walimuomba Mhe Mkuu wa wilaya aendelee na utaratibu wa kuwafikia wananchi kuwasikiliza Kero zao .
Naye Diwani wa Kata ya Ntobeye Mhe Sunday Mukozi Alimshukuru mkuu wa wilaya na timu yake nzima Kwa kuanzisha Kampeni kabambe ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Ziara ya Kutembelea Kata Kwa Kata inaendelea kesho tarehe 21/11/2023 Kwa Kata ambazo Bado .
Kauli Mbiu "ukiwa na kero tutakukuta katani kwako tutakusikiliza na kukutatulia"
Wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara kijiji cha Chivu ,Kigina Kata ya Ntobeye Wilayani Ngara
Wataalam wa Halmashauri wakisikiliza Kwa makini kero zinazofolewa Ili kuzitolea ufumbuzi/utatuzi
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa