- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA
Leo tarehe 7/12/2023 Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe.Kanali Mathias Julius Kahabi akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji ndg. Solomon Kimilike, OCS wa Rusumo, Mhandisi wa Ujenzi, Afisa Mipango, Afisa kutoka ofisi ya DSO, Mtendaji wa Kijiji cha Rusumo na Mwenyekiti wa Kijiji Kwa lengo la kukagua kazi ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za wananchi ambazo ziliharibiwa na milipuko ya baruti, wakati wa Ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia maji kupitia Benki ya Dunia.
Mhe. Mkuu wa Wilaya akiwa na timu yake walifanya ukaguzi wa kampuni mbili za wakandarasi ambazo ni Azhar Construction Co.LTD na Kika Construction Co.ltd.
Mapungufu yaliyobainika ni nyumba kutojengwa kwa viwango vinavyotakiwa, mfano. Vipimo kutofuatwa ipasavyo, udongo wenye rutuba kutoondolewa na kuweka changalawe ambayo imechaguliwa, kuweka plastic sheet juu ya jamvi badala ya kutumia DPC ili kuzuia maji kupanda kwenye ukuta, kutofunga Joints wakati wa kujenga mawe ipasavyo hali ambayo itaruhusu nyufa kutokea kipindi kifupi kijacho ukizingatia ukanda wa mkoa wa Kagera unaathirika na tetemeko za mara kwa mara.
Aidha waliona hata kutofunga linta ya usawa wa Madirisha kuzuia nyufa kwa sababu tofali za blocks hazistahimili misukosuko ya mitetemo mbalimbali hivyo nyufa hutokea katika majengo.
Mhe. Mkuu wa wilaya ameelekeza timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kuundwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa kazi zote zinazoendelea na wakandarasi ili ziwe kwenye ubora unaotakiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara akikagua ujenzi usiokuwa wa viwango na kukataa ubabaishaji huo unaofanywa na wakandarasi.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J. Kahabi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike wakiwa wananyeshewa mvua kubwa iliyonyesha.lakini kazi ya Ukaguzi iliendeleaa.
Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Julius Kahabi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike pamoja na wataalam na viongozi Mbalimbali wakiwa wameloa mvua kubwa kuwanyeshea lakini kazi ilifanyika ya Ukaguzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi aliendelea kukagua akiwa na Mkugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike pamoja na wataalam, viongozi mbalimbali alifuata nao Kijiji Cha Rusumo.
Iwe Mvua iwe Jua kazi iendeleee Mkuu wa Wilaya Mhe.Kanali Mathias Julius Kahabi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon Kimilike.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa