- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael M. Mtenjele amewaagiza mawakala wanaonunua kahawa kwa wakulima ikiwa bado shambani kuacha tabia hiyo badala yake ivunwe na kuuzwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali.
Ametoa agizo hilo wakati akifunga kikao cha maadalizi ya ujio wa Mwenge wa uhuru kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Amesema tabia ya kununua kahawa ikiwa shambani kunawanufaisha walanguzi kuliko wakulima kwani mkulima akiishauza kahawa hiyo hana mamlaka nayo tena.
Akasisitiza kuwa serikali ipo kuhakikisha kuwa kila mkulima ananufaika na matunda ya jasho lake na wala hadhulumiwi. Kutimiza azma hiyo amewaagiza watendaji kata na vijiji kukomesha tabia hiyo na kuwataka wamletee majina ya watakaokaidi agizo hili.
Kwa wale waliokwishanunua kahawa hiyo Mkuu huyo wa wilaya amesema hawaruhusiwi kuivuna badala yake watafute njia ya kurejeshewa fedha yao. Ameahidi kutuma timu vijijini itakayohakikisha kwamba kila mkulima anavuna kahawa yake na kuiuza kwa utaratibu uliopangwa na serikali.
Aidha, amezitaja kata zinaongoza kwa kuuza kahawa iliyoko mashambani kuwa ni Kanazi, Kirushya na mabawe na kuwaonya kuacha tabia. Amemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Ndg. Aidan John Bahama kuwaandikia walanguzi hao barua ili waelewe kuwa wanachokifanya si sahihi na hakikubariki. Hata hivyo, walanguzi hao wametakiwa kufika ofisini kwa mkuu wa wilaya ili waweze kuongea naye kwa lengo la kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kwa watakaokaidi agizo hili.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa