- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias Kahabi amewapongeza na kuwashukuru viongozi mbalimbali kwa ushirikiano na upendo wa hali ya juu kuungana pamoja na kufanikisha zoezi la usafi siku ya Alhamis tarehe 16/11/2023 wilayani Ngara.
Mkuu wa Wilaya amewataka waendelee na moyo huo bila kuchoka na bila kumwacha hata mmoja nyuma.
Mkuu wa Wilaya alisema Tulianza kidogo kidogo zoezi la Usafi lakini sasa hivi gari limewaka na wote tunatembea pamoja hongereni sana .
Mkuu wa Wilaya Rai yake ni kwamba usafi huu sasa uwe endelevu kila asubuhi Kiongozi kabla hajafika ofisini kwake kuwe na tabia na utamaduni wa kukagaua kwanza mazingira yetu na maeneo yote ikiwemo Mitaa na Vitongoji Vyetu, Barabara na Mitaro yote, center zetu za Barabarani na pembeni mwa Barabara, maeneo ya ofisi zetu na majumbani kwenu na kwa Wananchi wetu pamoja na Vizimba pia vyoo kwa Wananchi wetu kuhakikisha wananchi wetu wana vyoo kila kaya pia kila nyumba.
Mkuu wa Wilaya alisisitiza maeneo ya biashara kwenye magulio/masoko/minada na meneo yote ya biashara. Viongozi tunaohusika kusimamia hali ya usafi wa mazingira na afya zetu kwa ujumla pia aliwapongeza Ndg Mansour Kalokola na ndg Yasini S Mwinoli kutoka ofisi ya afya.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa