- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael M. Mntenjele ametoa mchango wa mabati mia moja( 100) yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili na laki nane (2,800,000/=) katika shule ya msingi Ruhuba iliyoko kata ya Mbuba wilayani Ngara. Wakati akikabidhi mabati hayo mbele ya wananchi na kamati ya shule ya ujenzi, Mkuu wa wilaya alisema kuwa ameona ni vema kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi huo waliouanza baada ya kuridhishwa na juhudi ambazo zimefanywa na wanachi wa kata hiyo. Pia alitoa wito kwa wananchi kushirikiana pamoja pale linapotokea jambo ambalo litahitaji mchango wao ili kulifanikisha maana ni kwa ajili ya wanaufaa yao na vizazi vyao pia.
Mkuu wa Wilaya aliwaomba pia wadau mbalimbali kujitokeza na kuwaunga mkono wananchi ambao wanaonesha juhudi zao binafsi katika kutatua changamoto zao mbalimbali katika jamii.
Nae mwananchi wa kijiji cha Ruhuba,ndugu Yahya Rashidi alitoa shukrani zake kwa Mkuu wa wilaya kwa msaada wa bati alizotoa na kusema kuwa msaada huo utakuwa ni hamasa kubwa kwa wananchi na umewapa nguvu kubwa ya kuendelea kuchangia ili waweze kuukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo.
Mkuu wa shule ya Ruhuba alitoa pongezi zake kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuunga mkono juhudi za wanachi na kuahidi kuukamilisha ujenzi huo ndani ya muda waliojipangia na wananchi ili wanafunzi waweze kupata sehemu za kusomea na ofisi za walimu ziweze kupatikana.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa