- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe. Kanali Mathias Julius Kahabi, amefanya ziara kukagua Mradi wa Maji. Pia kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Rusumo.
Mkuu wa Wilaya katika Ziara hiyo akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Mhe Wilbard Bambara Diwani Kata hiyo ambaye ni Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya, Kamati ya usalama, Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na viongozi wa Kata hiyo.
Mkuu wa wilaya na timu yake wametembelea mradi mkubwa wa Maji Rusumo ambao umegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 3.04 ambao umekamilikana Sasa upo kwenye majaribio.
Pia Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanali Mathias Kahabi amefanya Mkutano wa kusikiliza kero Kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Rusumo. Wananchi hao ambao nyumba zao ziliathiriwa na mlipuko wakati wa utekelezaji wa Mradi wa umeme.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe. Kanali Mathias Kahabi aliyesimama akiwa na Mkiti wa Halmashauri Mhe. Wilbard Bambara, kamati ya usalama na wataalam Kutoka Halmashauri na Taasisi mbalimbali katika zoezi la kusikiliza kero na uongozi wa Kata ya Rusumo
ssMradi mkubwa wa Maji Rusumo
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa