- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika Ujenzi wa Jengo la Halmashauri makao mkuu na kuridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi huo.
Katika ukaguzi huo Mhe Kanali Kahabi alipata maelezo ya kina toka kwa Msimamizi Mkuu Mkuu wa Ujenzi huo Injinia Emmanuel na kueleza kuwa Ujenzi umefikia asimia 84 na kutarajiwa kukamilika mapema Mwezi September.
Aidha, Mhe Kanali Kahabi amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri *Ndg Solomon Kimilike* na timu ya Wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa usimamizi mzuri unaendelea katika Ujenzi huo.
Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Mkurugenzi pia amempongeza Mkandarasi ambaye anafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamilika mapema iwezekanavyo.
Ngara Kazi inaendelea.
Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara alipotembelea ujenzi wa Jengo la ofisi ya Halmashauri Makao Makuu .
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa