- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya Ngara ametoa Motisha ya Tsh 50,000/ kwa Mshindi wa usafi kwa mwezi Desemba 2023 ambapo Ndg Japhet Jakob Sulisaho - Mtendaji wa Kata ya Murusagamba ameibuka Mshindi na kukabidhiwa Motisha hiyo.
Motisha imetolewa mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya katika Ukumbi Mdogo wa Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Ndg Solomon kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngara amempongeza Mtendaji huyo kwa umahiri wake wa kusimamia shughuli za usafi na utunzaji wa Mazingira pamoja na usimamizi wa shughuli za Serikali katika eneo lako.
Zoezi hili Kutoa Motisha ambalo ni chachu Kwa watendaji wa Kata lilianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanali Mathias J. Kahabi tangu mwezi Novemba ambapo Mtendaji Kata ya Rusumo alikabidhiwa Motisha hiyo.
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mathias J. Kahabi aliye katkati baada ya kukabidhi Motisha ya usafi ambapo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike akimpa mkono wa pongezi Mtendaji wa Kata ya Murusagamba , aliyepo kushoto ni Katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani Ally Lukali.
Katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani A.Lukali akimpongeza Mtendaji wa Kata baada ya kukabidhiwa Motisha ya usafi na Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J.Kahabi aliye katikati na aliye kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa