- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wataalamu wanaosimamia mradi wa umeme wa maji wa Regional Rusumo Falls Hydroelectric Power (RRFHP), uliopo Rusumo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kukamilisha mradi huo ifikapo ifikapo 2020 kadiri ya mkataba unavyosema.
Waziri wa Nishati Mh. Dr. Medard Kalemani wa Tanzania, na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Balaozi Claver Gatete, wamefikia uamuzi huo Juni 09, 2018, baada ya kutembelea eneo la mradi na kujiridhisha kwamba kazi inaendelea vizuri ingawa bado kuna changamoto.
Mawaziri hao wamewashukuru wataalamu hao, kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha mradi huo, unakamilika kwa wakati inagawa wataalamu, wangependa mradi ukamilike ifikapo mwaka 2022.
Waziri wa Nishai wa Tanzania Mh. Dr. Kalemani, amekataa kuongeza muda kwa madai kwamba haoni sababu ya kuongeza muda huo, kwani miezi iliyobaki inatosha kukamilisha mradi huo ikiwa watajituma.
Aidha, amewataka wataalamu kuonyesha ushirikiano na wenyeji wa Rusumo kwani bila wao mradi huo, unaweza kukwama, na kwamba kila watakapokuwa na vikao wawashirikishe wananchi hao, kwani mradi humo katika eneo lao.
“Mjenge mahusuiano mazuri na wananchi kwa sababu bila kufanya hivyo, shughuli zenu zitasusua, hata hivyo, inabidi mradi huo kama wao na kazi zenu zitaendelea bila matatizo yoyote.” Alisema Dr. Kalemani.
Mh. Dr. Kalemani amewataka wataalamu hao kushikiana na wenyeji, baada ya wananchi hao kuuzuia msafara wake kwa madai kuwa wataalamu wa mradi huo wanawabeza, kuwadharau na kuwatenga katika shughuli zao ikiwemo ajira.
Waziri Dr. Kalemani aliwataka wananchi hao kuorodhesha hoja zao za msingi na kuzikabidhi kwa kiongozi wao, ambaye ataziwasilisha kwenye vikao vya wafanaykazi wa mradi wa Regional Rusumo Falls Hydroelectric Power (RRFHP), kwa ufumbuzi wa matatizo yao.
Naye waziri wa Miundimbinu wa Rwanda Balozi Gatete, aliwashukuru wataalamu wa mradi huo, na akataka kujua iwapo matengenezo hayo, hayataathiri barabara inayopita katika eneo la mradi huo.
Wataalamu walimuhakikishia kuwa wamekwishafanya tathimini kuhusu usalama wa barabara, na kwamba barabara hiyo iko salama, na hata Miundombinu mingine, inayoizunguka mradi huo ahuna madhara dhidi yake.
Mradi wa Regional Rusumo Falls Hydroelectric Power (RRFHP), ukikamilika utakuwa na uwezo wa kutoa MW 80, ambazo kila nchi itapata MW 26.7.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa