- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mradi wa umeme wa maji wa Rusumo kupitia mradi wa Local Areas Development Projects (LADP), unatarajia kutumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 5, kufadhiri miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Willaya ya Ngara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amesena hayo June 27, 2018 ofisni kwake, kwamba miradi hiyo itahusu huduma za afya, elimu pamoja na kilimo.
Amesema miradi hiyo inatolewa katika maeneo yaliyozungukwa na mradi mkubwa wa umeme wa Rusumo, ambapo kwa Tanzania wilaya ya Ngara itanufaika na mradi huyo; huku Burundi na Rwanda watakuwa na miradi ya aina hiyo hiyo.
“Katika wilaya yetu ya Ngara mradi huu tunaupokea kwa mikono miwili, kwani una miradi miwili mikubwa itakayofanyika katika wilaya yetu; wa kwanza ni wa kwa wale wananchi walioathiriwa na mradi wa umeme wao wana miradi ambayo itawainua kiuchumi.” Alisema Ndugu Bahama.
Alitoa mfano wa miradi ya kiuchumi kuwa ni ufugaji, kilimo katika Nyanja ya kahawa pamoja na kujengwa chuo cha ufundi cha Lemera, maji na ile ya afya; na kwamba fedha yote inatolewa na Benki ya Dunia.
Mradi wa pili ni ule wa dola za kimarekani milioni 5, ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu hadi unakamilika, na kwamba wamekwisha pokea zaidi ya shilingi milini 300 za kitanzania, kwa ajili ya kutekeleza mradi huo tangu Juni mwaka 2018.
Mkurugenzi huyo Mtendaji Ndugu Bahama, amefafanua kwamba shilinig milioni 300 alizopkea ni za kuanza kutambua miradi mbalimbali itakayowanufaisha wananchi, na kwamba vipaumbele vinaelekezwa katika huduma za maji, kilimo, afya pamoja na elimu.
Amefafanua kwamba vijiji vitakavyopedelea kujihusisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, vimetengewa dola za kimarekani zipatazo $162,000, ambazo zitatumika kutoa elimu ya ufugaji kwa wananchi pamoja na kuwanunulia ng’ombe wakuanzisha mradi huo.
Hata hivyo, ametoa mfano kwamba kwa wale wananchi watakaotaka kufuga nyuki, kwa ajili ya kuzalisha asali; hao wametengewa dola za kimarekani zipatazo $91,000, Miradi mengine iliyotengewa fedha ni miradi ya kilimo dola $209,000, miradi ya maji $2,210,000.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa