- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mawaziri wanaosimamia mradi wa ujenzi wa umeme wa megawati 80 katika maporomoko ya mto Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda, limeagiza bodi ya wakurugenzi wa mradi huo, kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ifikapo Februari 13, mwaka 2020.
Waziri wa Nishati wa Tanzania Medard Kalemani, akiongozana na waziri wa Nishati na Madini wa Burundi Mhandisi Come Manilakiza, na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Balozi Clever Gatete wametoa wametoa agizo hilo February 4,2019 wilayani Ngara mkoani Kagera, walipokutana kukagua ujenzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa baraza hilo Medard Kalemani, amesema lengo la kukutana katika mradi huo, ni kukagua ujenzi wa bwawa la kuzalisha na kusafirisha maji , nyumba za watumishi, jengo la kuzalisha umeme, na kuweka mikakati ya kuharakisha ujenzi, kisha kubaini changamoto zinazokabili mradi huo.
Kalemani amesema baada ya kutembelea mradi huo, ulioanza mwaka 2015, ukisainiwa na aliyekuwa waziri wa nishati na madini wa Tanzania Profesa Sospiter Muhongo, wameridhishwa na maendeleo ya mradi huo, lakini wakawataka wakandarasi kuongeza nguvu zaidi ukamilike haraka.
“Wataalam wamazie kazi zao, kwa kuzifanya kitaalam, masuala yanayohusu mamlaka bodi ya wakurunzi na na wataalam, washirikishe mamlaka zilizo juu yao, ilituweza kukamilisha mradi huo kwa wakati, na kunufaisha wananchi wa nchi zetu.” Amesema Kalemani
Benki ya Dunia kupitia bodi yake ya utendaji, ilidhinisha dola Milioni 340 za kimarekani, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo mkubwa, kwenye maporomoko ya mto Rusumo ulioko mpakani wa Tanzania na Rwanda, utakaowanufaisha wakazi wapatao milioni 62.
Hata hivyo, Mawaziri wa Nishati kutoka nchini Burundi na Rwanda, wamewataka wakazi wa mataifa hayo, kuongeza uzalishaji mali jirani na mradi huo, ili kupata mali ghafi zitakazohitajika katika viwanda, vitakavyotumia umeme huo; huku wakinufaika na reli kutoka Isaka kwenda mataifa hayo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa