- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mashindano ya kuibua vipaji Kwa wasanii wa kuimba Wilayani Ngara (Ngara star Search) yalianza tarehe 24/02/2024 washiriki wakiwa 31 Kutoka Kata Mbalimbali za Wilaya ya Ngara., ambapo mzunguko wa pili uliofanyika 09.03.2024 Kwa washiriki 14 walifanikiwa kuingia mzunguko wa pili na kubaki washiriki 7 walifanikiwa kuingia Hatua ya fainali .
Mashindano hayo yaliyofanyika Malaika Beach Mamlaka ya mji Mdogo Rulenge yaliyoratibiwa na Mc Oswald Madard Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Ofisi ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya aliyewakilishwa na Ndg. Mugisha Rubagora, pia Makamu Mkiti wa Halmashauri Mhe. Adronizi Bulindori Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri aliyewakilishwa na Ndg Said Salum, Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Ngara Mhe Fabian Niyonzima Diwani Kata ya Rulenge , Ndg Privanus Katinihila Mkuu wa Idara ya Biashara viwanda na uwekezaji , Bi Elina Patrice Utamaduni Sanaa na Michezo , viongozi wa Chama na serikali.
pia wadhamini walihudhuria ambao ni NMB, Ngara oil, Barikiwa Motel, mama kervin,Classic wear,mama linet Beauty saloon, mnema microfinance Ltd. Aidha uongozi uliwashukuru sana wadau wote pia walimshukuru Mhe Oriva Semuguruka Kwa support ya Redcapet, na Mhe Ndaisaba Ruhoro Kwa Kutoa zawadi za mshindi wa kwanza , wa pili na wa tatu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. solomon Kimilike Kwa Kutoa Magari na mafuta Kwa ajili ya ufuatiliaji tangu maandalizi ya mashindano yaanze Kwa Maafisa.
Washiriki walikuwa Saba na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Mshindi wa 1 Hadi 3 walipatiwa zawadi fedha taslimu na Mgeni rasmi , kurekodi nyimbo Number one Bure.
Majaji walikuwa wanne wakiongozwa na Chief Judge Ndg. Lucas Magale Mkurugenzi wa Number one production.
Mhe Adronizi Burindoli makamu Mkiti wa Halmashauri akiwa na Mhe Fabiani Niyonzima Diwani Rulenge kabla ya mashindano ya kuibua vipaji vya Sanaa kuimba Malaika Beach Rulenge.
Washindi watatu wakiwa na wadau mbalimbali baada ya mashindano kumalizika.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Ndg Mugisha Rubagora akiwa na Washindi pamoja na viongozi Toka Halmashauri pamoja na Mc Oswald.
washindi watatu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkiti Uvccm Cde Hakiza.
Washindi wakiwa na viongozi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa