- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wapatao 4,643 wa Mamlaka ya Mji wa Ngara, wananufaika na huduma ya maji safi na salama, baada ya mtambo mpya kununuliwa na kusimikwa.
Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Simeon Ndyamukama, ameyasema hayo ofisini kwake Machi 26, 2018; kwamba mtambo huo unazalisha wastani wa lita 215,000 za maji kwa siku.
“Maji yanayozalishwa na mtambo wetu mpya, yanawahudumia wananchi na taasisi katika maeneo ya; Murgwanza, Mukanywampezi, Mukididili na Mukirehe.” Alisema Ndyamukama.
Amesem hadi unakamilika mradi huo wa maji, umeghalimu jumla ya shilingi 21, 769,180/=, ambazo zilitumika kwa ajili ya kununua na kuufunga mtambo huo.
Ameogeza kwamba Mhe. Rais alitoa shilingi 13, 000,000/=, kununua mtambo huo kufuatia kilio cha wananchi, waliotaka kupata huduma hiyo baada ya mtambo uliokuwepo kuharibika.
Kwa upande mwingine, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilichangia jumla ya shilingi 8,769,180/=, ili kufanikisha ununuzi na ufungaji wa mtambo huo.
Aidha, amesema mtambo huo umenunuliwa, kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli aliyoifanya wilayani Ngara Julai 2017.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa